Rayvanny - Unaibiwa Lyrics


(Verse 1)

Usidate na njonjo za mapenzi

Vicheko bandia Usoni Kudeka Kumbe Ana pretend

Maufundi toka Tanga na Zenji

Vionjo Mitego Unase ashike pochi Umwage chenji

Anakuchanganya kiunoni shanga

Marashi Kama Uko peponi

Mtoto Sauti Kinanda

Ya kumtoa chatu pangoni

Ukishatafuna Karanga

Hutaki hata Aende Sokoni

Anakuchuna Mafaranga Unabaki Na Vumbi Mfukoni


(Pre Chorus )

Ukiwa Na pesa Utasifiwa Kitambi

Baby Me I like that

Nakukupamba Kwenye Simu Video Snapchat

Kumbe Hana Maana Hadi Mangi

Anamwita Sweetheart

Kisa Anakesha Gym kutafuta Six packs


(Chorus )

Unaibiwa!! Unaibiwa!!

Unaibiwa!! Unaibiwa!!


(Verse 2)

Kuna Kina Rose Visosa

Wale Wapenda Verossa

Ukipita Na shati Na Moka

Lazima Watashoboka

Wakiomba Lift Ogopa

Miguu dashboard Vishoka

Mchunguze cheni Goroka

Nywele Na pochi kakopa

Eh

Usije Kuyavamia Yasije Yakakutesa Hawachelewagi Kukimbia

Kuna Wenzako wanalia walizani Mapenzi pesa Kwenye Suruali Vibamia

Hata Ukimuonga Ferrari Hatokuona Rijali

Wakati chumbani we Beki Ukifunga Moja Tu chali

Atakamatwa Na mangangali

Vijana Machachali

Hawachagui sehemu Ya Vita Uvunguni Na juu Ya Dali


(Pre Chorus )

Ukiwa Na pesa Utasifiwa Kitambi

Baby Me I like that

Nakukupamba Kwenye Simu Video Snapchat

Kumbe Hana Maana Hadi Mangi

Anamwita Sweartheart

Kisa Anakesha Gym kutafuta Six packs


(Chorus )

Unaibiwa!! Unaibiwa!!

Unaibiwa!! Unaibiwa!!


(Bridge)

Unadhani Niwapekeako

Kumbe wengine Wameshaweka Kambi

Kakupendea Macho

Wapo wengine kawapendea Rangi

Ye ni gari la dampo

Hachagui Taka dereva Mpe Ganji

Wakubadili sample

Akila Mihogo Karoti Hazipandi


(Chorus)

Unaibiwa Unaibiwa

Unaibiwa Unaibiwa