Diamond Platnumz Kosa Langu

Kosa Langu

Artist : Diamond Platnumz

Album : A Boy From Tandale

Release at : 14 Mar 2018

Diamond Platnumz Kosa Langu Lyrics

[VERSE 1]

Barua yako uliyotuma

kwa Ricardo Momo nimeisoma

Ila nimechelewa kuijibu

Sababu moyoni imenchoma

Nliyo yategemea

Tofauti na nlicho kiona

Hata naandika hii barua

Huku roho yangu inansonona

Umesema nichane nguo

Pia funguo umeirudisha sawa

Simu niziweke kituo

Na sio chaguo

Nikome kabisa sawa

Umesema hata ile picha nzuri

Nliyo kukumbatia

Niichane sawa

Ila kinachoniumiza

Mbona moja umesahau


[CHORUS]

Kosa langu kosa langu hujaniambia

Na kuniacha peke yangu ukanikimbia

Ila mbona kosa langu hujaniambia yeaaah

Nami nikabiki peke yangu ukanikimbia


[VERSE 2]

Mbona ukanichimbia kaburi ningari bado mzima

Niife nizikwe vizuri nipotee kabisa kimya

Licha ya matendo mazuri kwa upendo na heshima

Moto ukachochea tanuri ukachoma wangu mtimaa

Natamani hata ningepata nafasi

Muda wakati Kukutazama

Unione hata japo sura

Unitazame macho yangu mwenzako wimbi

limenipiga kasi

Langu jahazi limezama

Mnyonge mwana Sanura

Wee ndio ulikuwa furaha yanguTatizo hata nkilia

Wa kunifuta machozi sina

Sawa na gari lisio na gear

La kuiforce ipande mlima

Ndio maana siishi kulalama

Japo jibu moja tuu

Linaloniumiza mwenzio bado sijaelewa


[CHORUS]

Kosa Langu kosa langu (Kosa langu)

Hujaniambia (Hujaniambia)

Na kuniacha peke yangu (peke yangu)

Ukanikimbia (Ukanikimbia)

Ila mbona kosa langu (Kosa langu)

Hujaniambia  (Hujaniambia)

Nami nikabiki peke yangu (Peke Yangu)

Ukanikimbia (Ukaenda Ooh!)Wasafi Records


(Oooh moyo)

Moyo wangu umevunjika una magongo

(Oooh moyo)

Kila sehemu nayoshika kinyamazongo

(Oooh moyo)

Hata chozi likifutika linabaki tongo

(Ooooh moyo)

Najitahidi kulidhika ila nna kinyongo


(Ooooh moyo) Moyo wangu umevunjika Unaa jamani

(Ooooh moyo) Hhhhmm hmm