Aslay Bye Magufuli lyric

Bye Magufuli

Aslay Aslay
25 March 2021
35

Aslay Bye Magufuli Lyrics

We mwana Chato we

Ona wenzio tunavimba macho kwa kulialia

We mwana Chato we

Hivi ni kitu gani tueleze tuchokufanyia


Mwanachato mbona ulitupenda

Nasi tulikupenda pia

Mwanachato ee, Mwanachato

Kipenzi cha Tanzania na dunia pia


Mama Janet we ngoja kitambaa

Nitafute nikufute nyamaza kulia

Kiatu chako wee, hakuna atayekivaa

Mbingu ardhi ipasuke unavyoumia


Kufa usifiwe, ishi uzomewe

Magu mi bado sijatosheka

Magu amka hata nusu dakika

Mungu tusamehe tulipokosa

Magufuli bado tunamtaka


Bye bye, bye bye

Bye bye Magufuli wetu

Bye bye, bye bye

Bye bye Magufuli, tutaonana tu


Ulitaka tuishi kwa mfano

Ulipenda amani ulipenda muungano

Masikini ukatupa somo

Tunaishi kwa kunata ulitupa mdomo


Oh mchanga umemeza

Viongozi waloweza

Hata hukumaliza Magu wewe

Wasalimie eeh, Nyerere Karume

Kabasefu wee na wengine


Jembe, Magufuli jembe

Kwaheri bwana John Pombe

Jembe, Magufuli jembe

Kwaheri Rais wa wanyonge


Kufa usifiwe, ishi uzomewe

Magu mi bado sijatosheka

Magu amka hata nusu dakika

Mungu tusamehe tulipokosa

Magufuli bado tunamtaka


Bye bye, bye bye

Bye bye Magufuli wetu

Bye bye, bye bye

Bye bye Magufuli, tutaonana tu
Comments

You may also like these lyrics

00:00 00:00