Diamond Platnumz Acha Nikae Kimya lyric

Acha Nikae Kimya

Diamond Platnumz Diamond Platnumz
18 March 2021
55

Diamond Platnumz Acha Nikae Kimya Lyrics

Mmmh mmmh

Mama ananiambia Nasibu

Mimi ni mtu mzima na we ndo nakutegemea

Yanayotokea jaribu kupiga kimya

Usidiriki hata kuongea


Mara nasikia vya aibu

Konda Gwajima eti ugomvi umekolea

Kuchunguza karibu

Ni binti mmoja kwa mitandao anachochea


Najariibu kunyamaza, ila moyo utaki

Unaniambia eti Simba japo nguruma uisemee haki

Oooh najaribu kunyamaza hata Laizer hataki ooh

Anasema walau nena kidogo


Na mashabiki Dangote

Wananiambia mbona husemi chochote

Aah si uko nao siku zote, ama ulezi unafanya uogope

Aah na media pande zote wanalalama kiongozi Atoke

Nchi inaingia matope

Niende wapi na mi mtoto wa wote


Acha nikae kimya (nisiongee)

(Kimya) ooh ninyamaze mimi

Nikae kimya, nisiseme (kimya)


Mama kanambia (wacha nikae kimya)

Oooh nifunge mdomo (kimya)

Mie bado mdogo sana (kimya), nisiseme (kimya)


Mmmh ni mengi majaribu najitahidi epuka yasijeni-cost

Japo mengine swadakta mengine hayana maana

Rafiki kipenzi wakaribu ata nyimbo yake sikueza ipost

Ila alivokamatwa iliniumiza sana


Mitandao kila kona

Uongo na ukweli unashonwa

Kila nyumba inanongona

Aaah Ooh Tanzania


Mara kimbembe Dodoma

Bunge wapinzani wameg'oma

Juzi akapotea na Roma

Ooooooh Tanzania ooooh


Najariiibu kunyamaza

Makame hataki oooh eh

Ananiambia walau nena kidogo


Nyumbani nafungua geti

Niende kwa mangi nunua spaghetti eeh

Napewa za chini ya kapeti

Kuna redio imevamiwa eti


Eeh napita kwenye magazeti

Nakuta rundo la watu wameketi eeh

Badala ya kutafuta senti

Wanabishana tu mambo ya vyeti


Wacha nikae kimya (oh nisiongee)

(Kimya) ninyamaze kabisa (nikae kimya)

Ulimi koma (kimya)

Usijekuniponza (wacha nikae kimya)


Nifunge bakuli langu (kimya)

Nikojoe nikalale (nikae kimya)

Me bado mudogo sana (kimya)

Mama kanambia


Ooooh najiuliza (wapi)

Najiuliiza (wapi)

Tunakwenda wapi (wapi)

Kila siku maneno (wapi)

Ah tuacheni jamani (wapi)


Me na we ni taifa moja (wapi)

Kambarage baba mmoja (wapi)

Sa tofauti za nini tushikamane (wapi)

Tukaijenge Tanzania




Comments

Other song(s) of Diamond Platnumz

Diamond Platnumz
Diamond Platnumz
Diamond Platnumz
Diamond Platnumz
Diamond Platnumz
Diamond Platnumz

You may also like these lyrics

00:00 00:00