Harmonize Mpaka kesho Lyrics, Paroles

Mpaka kesho

20 July 2020
268

Harmonize Mpaka kesho Lyrics

Hello, Hello baby

Mmmh mmmh


Natamani niandike barua, na niitume kwako

Ilanahisi hutaisomaa, utaikataa

Hata simu nitajisumbua, kupiga namba yako

Maana hata ukiiona utaikata


I wish yawe ndoto, haya ninayo yapitia

Ama nirudi utoto imenisonga dunia

Eti kurwa bila ndoto, hivi ni wapi ntaanzia?

Kulia bila kushoto, sijawai kusikia


Eeh, imagine siwezi kukuota (aah aah aah)

Maana ata usingizi sina (Sinaa)

Mwenzako wataniokota (aah aah aah)

Maji yamenizidi kina (Mwenzenu mimi)

Mpaka kesho, eeh eeh

Mpaka kesho, umeniganda mawazoni

Mpaka kesho, bado nakuwazaa

Mmh mmh eeh

Yaani mawazo kizunguzungu (Mpaka kesho)

Insta napaona pachungu (Mpaka kesho)

Mateso nihurumie (bado nakuwaza)


Nishajaribu kudanga nipoteze mawazo, huenda nitaenjoy

Kumbe najivua utu na heshima

Kwa watabibu waganga

Nijue nini chanzo, mwenzako nipo hoi

Ama nyota yangu butu, makali sina


Eeeh, zile nadhiri

Kwamba utaniweka moyoni zinajirudia

Mie ndio moja we mbili

Mbona sasa sikuoni, umenikimbia

Mie mwenzako ka sabuni kichelema

Siezi ata kupangusa ah ah

Jeraha la penzi nachechema

Sina furaha ata ya kunusa ah ah

Yaani umeniacha dillema

Siwezi kupanda kushusha ah ah

Yaani mapenzi vitaa, CCM na Chademaa

Firauni na Musa ah ah


Eeh, imagine siwezi kukuota (Aaah aah aah)

Maana ata usingizi sina (Sinaa)

Mwenzako wataniokota (Aaah aah aah)

Maji yamenizidi kina (Mwenzenu mimi)

Mpaka kesho, eeh eeh

Mpaka kesho, umeniganda mawazoni

Mpaka kesho, bado nakuwazaa

Mmh mmh eeh

Yaani mawazo kizunguzungu (Mpaka kesho)

Insta napaona pachungu (Mpaka kesho)

Mateso nihurumie, (bado nakuwaza)


Wa kumove on nitakuwa mie (oh siwezi)

Yaani ipite siku nisikufikirie (oh siwezi)

Kuku unfollow nitaweza mie? (oh siwezi)

Kwenye page yako nisichungulie eeh (oh siwezi)

Other song(s) of Harmonize

Trendings Lyrics

00:00 00:00