Ibraah Hayakuhusu lyric

Hayakuhusu

Ibraah Ibraah
14 April 2021
13

Ibraah Hayakuhusu Lyrics

Wewe, aah aah ah

Haukutaka kulea, wakati unalelewa

Lazima uvunjie watu wazima heshima

Punguza mazea unajifanya una-care

Wakati umemtelekeza Fahima


Achana na walokutangulia

Wakati kesho yako hujui itakwangukia

Unaweza Wasafi ukatimuliwa

Na Konde Gang ukaja kusign-iwa


Unashindana na mwanajeshi

Ambaye vita aliianza baba yako (Na hawezi)

Msalimie kipa la ndezi

Mwambie hata akikesha kwa sango (Hatuhami Mbezi)


Nyimbo kaimbiwa Kajala

Karauka na kupwita pwita

Acha papara aah wee

Naskia unachimba mikwara

Hauna chochote wewe buma chakula ah wewe


Mapenzi ya Konde na Kajala

Yanakuhusu nini kaka wee (Hayakuhusu)

Hata wakiongea video call

Na Paula lakini si mwanae (Hayakuhusu)


We njoo ukomae na muziki (Hayakuhusu)

Ona kina Chinga tunahit (Hayakuhusu)

Ah tumeanza jana hatushikiki (Hayakuhusu)

Umeona Sound from Africa haisikiki, imebuma wee...


Mambo ya kuhonga waandishi wa habari

Nyi mmezoea tunawajua

Hata Youtube zetu mnapochokonoa

Si tunawajua, tunawajua


Kama vipaji mnavyo, sa wivu wa nini?

Tufanye kazi na tusonge mbele

Kama vipaji mnavyo, na mnajiamini

Ya nini sasa kupiga kelele


Eeh akina Lokole, si wanawapost

Sababu ndio machawa wao, ndio machawa wao

Kila siku anawapromote

Leo asikose ladha, ooh ladha ooh


Ah chondelei mrudie Fahima ukamtunze mwanao

Yasiwe ya Mzee Abdul na Nasibu

Kumbuka kujinyima usimsahau mwanao

Baadae akutunze usije pata aibu


Mapenzi ya Konde na Kajala

Yanakuhusu nini kaka wee (Hayakuhusu)

Hata wakiongea video call

Na Paula lakini si mwanae (Hayakuhusu)


We njoo ukomae na muziki (Hayakuhusu)

Ona kina Chinga tunahit (Hayakuhusu)

Ah tumeanza jana hatushikiki (Hayakuhusu)

Umeona Sound from Africa haisikiki, imebuma wee...




Comments

You may also like these lyrics

00:00 00:00