Ibraah Mapenzi lyric

Mapenzi

Ibraah Ibraah
09 January 2021
72

Ibraah Mapenzi Lyrics

Ndo aaah...aah 

(Mr Simon)

Aya aah aah eh eeh ehh..


Amini unayempenda

Naye ana wake anayependa pia

Na siku zinakwenda aah


Na hata yule anayempenda

Naye ana wake anayemwita dear

Haya mapenzi mwana kwenda aah


Na ni yale yale mapenzi

Yalotesa mabibi na mababu hadi leo

Mie mwenzenu siyawezi

Ni bora uyashuhudie kwa mwenzio ama kwa video


Usione mtu analiaga

Ukadhani ni utoto

Mapenzi yana vingi vituko

Nyingi changamoto ona


Ukimpata anayekudhamini mna

Tulia na utunze yake heshima

Ujue ndo ukashazama kwa kina wewe


Ah we vipo kwa kuvumilia 

Lakini sio mapenzi

Mapenzi yanaumiza 

Mi ndio maana siyawezi


Vipo kwa kuvumilia 

Lakini sio mapenzi

Mapenzi yanaumiza 

Mi ndio maana siyawezi


Ah we penda unapopenda

Unapo amini kwamba amani ya moyo wako ipo

Na ukikosa unachopenda

Utapagawa bure atafanya matambiko


Na na hata ukipenda kweli

Hawezi jua sababu ni siri ya moyo wako

Hata kama ukifeli

Atapuuzia ili uteseke tu peke yako


Ngoswe kitovu cha uzembe

Ukipenda huoni

Na unayependa hajui

Hatambui kama ye ndo ako mbooni


Hata akisema amechoka

We zidi kumpenda hivyo hivyo

Maana mapenzi hayana mwenyewe aah


Unaeza ukaondoka

Ukaenda kupenda pengine

Napo ukakuta ndivyo sivyo

Ukajihisi una mkosi wewe aah


Ukimpata anayekudhamini mna

Tulia na utunze yake heshima

Ujue ndo ukashazama kwa kina wewe


Ah we vipo kwa kuvumilia 

Lakini sio mapenzi

Mapenzi yanaumiza 

Mi ndio maana siyawezi


Vipo kwa kuvumilia 

Lakini sio mapenzi

Mapenzi yanaumiza 

Mi ndio maana siyawezi


(Ibraah, Konde Music)

 Comments

You may also like these lyrics

00:00 00:00