Mbosso Karibu Lyrics

Ishafika saba sasa, tunakungojea

Imebaki miezi miwili tu, ebu siku sogea

Tuna shauku na bashasha, ya kukupokea

Sio mimi na mama yako tu, na bibi anakuombea

mmmmmmh....


Imani yangu inanituma, unanisikia baba yoo (baba yo yo)

Na furaha yangu dongo kumung'unya, anapobugia mama yoo (mama yo yo)


Mmh, gari li wazi wazi, kuwa muda usha tawakal

Natamani useme zawadi ila acha ninunue vigari

Oooh kuna shangazi kibiti kwa mzee kikali

Ukiota meno wataleta viazi ule mihogo uwe ngangali

Ule mihogo uwe ngangali


Kwanza nitakupa jina gani (tarara tarara raraara tarara)

Kwanza karibu duniani baba (tarara tarara raraara tarara)

Kwetu furaha isiyo kifani (tarara tarara raraara tarara)

ila kuna mengi duniani baba (tarara tarara raraara tarara)


Mmh, kwa furaha niliyonayo, ngechinja ng'ombe kwa tambiko

Ila baba yako uwezo sina, pokea uji kwa kijiko

Pokea mwanangu (ai yo yo)

Tena awape habari, waropokaji wapambe

We ni wangu wa halali, wasije zani vya nyange


Dunia ni mafuriko vua koti,

Wanadamu mioyo ya matope

Ukitukanwa, mwiko usiogope

Jikawe mwana wa Dangote


Ooh, wasimuone

Kimasomaso wasimuone

Wenye jicho la chuki wasimuone mwanangu

Kimasomaso wasimuone


Ooh, wasimuone

Kimasomaso wasimuone

Wenye jicho la chuki wasimuone mwanangu

Kimasomaso wasimuone

Other song(s) of Mbosso

Trendings Lyrics

00:00 00:00