Mbosso Yalah lyric

Yalah

Mbosso Mbosso
09 March 2021
95

Mbosso Yalah Lyrics

(Ayolizer)
Nimesadiki ya wahenga

Penzi lina raha yake

Mzigo kwa tenga

Ifaacho mtu chake


Denge nimekatwa ngenga

Ah umate mate

Najinyenga nyenga

Mao mao tate


Huwaga sioni

Ninavyoipanda milima

Ulimi sikioni

Mwili wote wanizizima


Mwenzenu sioni

Macho mawili yote sina

Tunaanza jikoni

Mpaka varandani twalilima


Yalah! yalah yalah, yalah yalah

Oooh yalah yalah yalah

Penzi limenizidia, yalah yalah

Ni kubwa, yalah yalah

Zito, yalah yalah, yalah yalah


Tungezaliwa zamani

Ningesema penzi togo

Tulinywe kibarazani

Tukitafuna maboga


Nimekipanda uani

Kibustani cha uyoga

Tukishiba biryani

Baby tule mboga mboga


Sasa polisi wa nini?

Nikikosa nikamate wewe

Mahakama ya nini?

Nikikosa nihukumu wewe


Penzi chupa la balindi

Tuligide baby hadi tulewe

Videge shorwe vya nini?

Kifaranga we nibebe mwewe


Huwaga sioni

Ninavyoipanda milima

Ulimi sikioni

Mwili wote wanizizima


Mwenzenu sioni

Macho mawili yote sina

Tunaanza jikoni

Mpaka varandani twalilima


Yalah! yalah yalah, yalah yalah

Oooh yalah yalah yalah

Penzi limenizidia, yalah yalah

Ni kubwa, yalah yalah

Zito, yalah yalah, yalah yalah




Comments

Other song(s) of Mbosso

You may also like these lyrics

00:00 00:00