Rayvanny Kofi (Mugufuli) lyric

Kofi (Mugufuli)

Rayvanny Rayvanny
18 March 2021
42

Rayvanny Kofi (Mugufuli) Lyrics

Kifo, kifo, kifo

Kifo, kifo, kifo



Nuru imepotea mbele hauoni (Giza)

Kila kona machozi masikitiko mmmh

Nafsi za nyon'gonyea huzuni moyoni

Unaumiza kitabu kizuri ndo kurasa ya mwisho

Vizuri havidumu

Nenda maguturi umetimiza majukuma, baba

Vizuri havidumu

Nenda jembe letu

Kuacha mabararara mahospitali

Wananchi ulivyo wajali

Masikini wakilali, Magufuli wetu

Upendo kwa wasanii kila mahali

Ulifurahi nasi

Ukatujali zile kofia kumbukumbu umefunga safari

Magufuli wetu


Kina mama atawafuta nani machozi

Wafungwa ulio wasamehe

Atawafuta nani machozi

Na vijana atatufuta nani machozi wazee wazee

Atatufuta nani machozi

Umeacha alama kumbukumbu isiyo futika

Pengo lako magufuli, sidhani kama litazibika

Moyo unalalama sisi bado twauzunika

Umefanya kazi ngumu shujaa

Bassi nenda kupumzika jembe leeeeeetu


Kifo, kifo, kifo

Kifo, kifo, kifo

Kifo, kifo, kifo

Kifo, kifo, kifo


Hauna huruma kwanini

Machozi mama Samia

Atayafuta nani

Machozi ya kasimu majaliwa

Atayafuta nani

Machozi ya bashiru

Atayafuta nani

Machozi ya polepole

Atayafuta nani

Machozi ya mama Magufuli

Atayafuta nani

Machozi ya watanza nia

Atayafuta nani






Comments

You may also like these lyrics

00:00 00:00