Rayvanny Nyamaza lyric

Nyamaza

Rayvanny Rayvanny
13 April 2021
17

Rayvanny Nyamaza Lyrics

Weka pombe sigara chini subiri tuongee

Zima kijiti marijuana za nini? Ngoja tuongee

Mbona ulisema mengi ukitaka nipotee

Sa umefanya nini? Na ulisema nini wala usijitetee


Macho hayana pazia

Nilimwona navutia

Naye kanikubalia

Kumbe moyoni unaumia


Dunia imejaa visanga

Ubinadamu umekuwa majanga

Tembo amefungwa kwa banda

Anataka kula kuku pia na vifaranga


Mungu tu akusamehe

Wewe ni kama ndugu yangu

Upunguze ma ugali

Uadui wa nini mwenzangu we


Ukitenda kosa na haujaomba radhi unakosea (Kosea)

Mama yake mzazi huruma ungemwonea (Mwonea)


Chunga kinywa kiwe na kituo

Hekima ndo iwe funguo

Maneno ya nini? Unajivua nguo

Kumbuka ulimwengu ni kama chuo


Ungenyamaza, bora ungenyamaza

Kaa kimya kama huna la maaana

Ungenyamaza, bora ungenyamaza

Ukikosa heshima bora kukaa kimya

Ungenyamaza, bora ungenyamaza

Bora ungenyamaza

Ungenyamaza tu, bora ungenyamaza

Kuwa muungwana


Mmmmh hasira hasara

Mimi ni ndugu yako kanitoa kafara

Ukakesha hukutaka kulala

Ukipambana niharibikiwe kaka wa Mtwara


Ukasahau mapenzi ni siri

Tena siri ya wawili

Kilichokuponza maadili

Tamaa ukashindwa isitiri


Tunza heshima yako

Na mashabiki wako hadi mbungeni

Na unapotongoza warembo

Boxer usiweke pembeni


Macho hayana pazia

Nilimwona navutia

Naye kanikubalia

Kumbe moyoni unaumia


Ukitenda kosa na haujaomba radhi unakosea (Kosea)

Mama yake mzazi huruma ungemwonea (Mwonea)


Chunga kinywa kiwe na kituo

Hekima ndo iwe funguo

Maneno ya nini? Unajivua nguo

Kumbuka ulimwengu ni kama chuo


Ungenyamaza, bora ungenyamaza

Kaa kimya kama huna la maaana

Ungenyamaza, bora ungenyamaza

Ukikosa heshima bora kukaa kimya

Ungenyamaza, bora ungenyamaza

Bora ungenyamaza

Ungenyamaza tu, bora ungenyamaza

Kuwa muungwana
Comments

You may also like these lyrics

00:00 00:00