Zuchu Utaniua lyric

Utaniua

Zuchu Zuchu
10 February 2023
12

Zuchu Utaniua Lyrics

Eti lah lah lah lalalala lala lalaah!

Lah lah lalalala lala lalaah!

Nna hamu mwenzenu nna hamu kuyahadithia

Oh nna hamu tena nna hamu kuyasimulia

Utani kama utani tulianza kimasiara

Sikudhani sikudhani yatafikia mahala

Akiwa hapatikani hapaliki sijalala

Kanifanya kitu gani mbona imekua mara

Dua la kuku menipata mwewe wallah nyinyi ni mtihani

Hata makosa ayafanye yeye mimi ndo naomba samahani

 

Ona anacheka kama mazuri

Anajua kabisa amenteka kwake sina shughuli

Eti kumwacha naanzaje sa kusepa natoa wapi jeuri

Na kwenye koma kaeka nukta kanitia na kufuriii

 

Oh! Baby mimi hapa taabani (wewe utaniuwa niuwa)

Nimeoza dah yarabi sihemii ( wewe utaniuwa niuwa)

Ah! Izo raha zakoo (wewe utaniuwa niuwa)

Roho yangu mali yako ooh (wewe utaniuwa niuwa)

Tukikosa stuli ni sunna kula kwenye mkeka

Unijue vizuri nikinuna mie ndo nadeka

Husijedhani kiburi uniache nikaja kuchekwa

Baby raha ya shughuli mkunwa awe na heka heka

Ooh husichokipenda wewe chunga na mimi husinifanyie

Mgomba wangu mwenyewe eti ndizi nigombanie

Nipe penzi nilewe umenizimiaa

Ooh ringa kwangu upo mwenyewe kiboko yangu miee Ooh vimbaa

 

Ona anacheka kama mazuri

Si anajua kabisa amenteka kwake sina shughuli

Eti kumwacha naanzaje sa kusepa natoa wapi jeuri

Na kwenye koma kaweka nukta kanitia na kufuriii

 

Oh! Baby mwenzako mimi twabani (wewe utaniuwa niuwa)

Chagua mwenyewe unizike unishafirishe ( wewe utaniuwa niuwa)

Ah! Izo raha zakoo (wewe utaniuwa niuwa)

Roho yangu mali yako ooh (wewe utaniuwa niuwa)




Comments

Other song(s) of Zuchu

You may also like these lyrics

00:00 00:00